18 Mei 2025 - 16:30
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan na Iran wamekutana na kufanya mazungumzo Mjini Tehran

Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya muda ya Afghanistan, ambaye yuko Iran kwa ajili ya kushiriki katika Jukwaa la Mazungumzo ya Tehran, amekutana na Sayyid. Araghchi na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa pande mbili, masuala ya kiusalama, hali ya wakimbizi na haki ya maji ya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (as) -ABNA-, Amir Khan Muttaqi, Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya muda ya Afghanistan, ambaye yuko nchini Iran kwa ajili ya kushiriki katika "Jukwaa la Mazungumzo ya Tehran", amekutana na kufanya mazungumzo na Seyed Abbas Araghchi.

Jukwaa hilo lilianza kazi leo (tarehe 18 Mei, 2025) kwa muda wa siku mbili katika Kituo cha Mafunzo ya Kisiasa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, likihudhuriwa na wajumbe 200 kutoka nchi 53.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya muda ya Afghanistan, katika mkutano huo walijadili kuhusu ushirikiano wa pande mbili, masuala ya kiusalama na hali ya wakimbizi wa Afghanistan walioko Iran.

Muttaqi alisisitiza juu ya kurudi kwa heshima kwa wakimbizi wa Afghanistan nchini mwao, na akatoa wito wa kuondoka kwao kwa hatua na kwa msaada wa Iran ili kuwawezesha kuishi tena nchini Afghanistan.

Pia alizungumzia suala la kuhamishwa kwa wafungwa wa Afghanistan walioko gerezani nchini Iran, akitaka masharti yawe rahisi zaidi kutoka kwa Iran kuhusu suala hilo.

Masuala ya kibiashara, usafirishaji kati ya nchi hizo mbili, na haki ya maji ya Iran kutoka Mto Helmand pia yalikuwa sehemu ya mazungumzo hayo. Muttaqi alisisitiza kuwa Afghanistan inaheshimu haki ya maji ya Iran na mkataba wa Helmand.

Haki ya maji ya Iran kutoka Mto Helmand imekuwa moja ya masuala muhimu katika mazungumzo ya viongozi wa nchi hizo mbili tangu kuanza kwa utawala wa Taliban miaka mitatu na miezi tisa iliyopita.

Ingawa upande wa Afghanistan unajiona kuwa umejitolea kwa mkataba huo, bado suala la haki ya maji ya Iran halijatatuliwa ipasavyo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha